Biko


Tangaza Hapa Ad

Michezo

Hatimae Yanga wameweka rekodi yao sawa uwanja wa Uhuru

on

Baada ya kuandamwa na kutofanya vizuri kwa club ya Dar es salaam Young Africans katika uwanja wa Uhuru ambao ndio wanautumia kama uwanja wao wa nyumbani, leo wamefanikiwa kupata ushindi mnono wa magoli 5-0 dhidi ya Mbeya City.

Game ya Yanga dhidi ya Mbeya City ilikuwa ni game ya tano ya Ligi Kuu kwa Yanga msimu huu kucheza katika uwanja wa Uhuru lakiniYanga ilikuwa haijawahi kupata ushindi wa zaidi ya goli 1-0 kwa michezo yake yote minne katika uwanja wa Uhuru.

Michezo yao minne iliyopita uwanja wa Uhuru dhidi ya Lipuli 1-1, Yanga 1-0 Ndanda FC, Yanga 0-0 Mtibwa Sugar na Yanga 1-1 Simba, hivyo hat-trick Obrey Chirwa (dakika ya 20, 50 na 59) pamoja na magoli ya mawili ya dakika ya 22 na 80 ya Emmanuel Martin yamevunja mwiko wa Yanga kutopata ushindi wa zaidi ya goli moja katika uwanja wa Uhuru.

Taarifa rasmi kutoka Ubelgiji, Samatta atafanyiwa upasuaji

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement