Tangaza Hapa Ad

AyoTV

VIDEO: Ufafanuzi alioutoa Zitto Kabwe kuhusu sakata la IPTL

on

Wakati mgogoro kati ya IPTL na benki ya Standard Chartered  ukiibuka upya baada ya mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa kibiashara ‘ICSID’ iliyopo nchini Uingereza kuitaka TANESCO kuilipa kwa niaba ya IPTL kwa sababu ilinunua deni la kampuni hiyo.

Taarifa zinasema kwamba IPTL imekata rufaa kwa wananchi kupinga uamuzi uliotolewa na ICSID wa kuitaka TANESCO kuilipa Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong BILIONI 320 na riba ya asilimia nne. 

Sasa leo October 6  2016 mbunge wa kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amekaa kwenye Clouds 360 ya clouds TV na kutoa ufafanuzi kuhusu suala la kampuni ya kufua umeme la IPTL na TANESCO, Zitto amesema………

>>>’Jambo hili ni suala la wizi, ni utapeli wa kimataifa, tulikuwa tuna fedha ziko benki kuu, sehemu ya fedha zinatakiwa kwenda kwa kampuni binafsi iliyotuuzia umeme, sehemu ya fedha zile zirudi TANESCO kwa sababu tumewalipa zaidi, mzizi wa fitina ndio ulipo hapo’

>>>’kila siku namuuliza Rais unatumbua majibu yote lakini hili la IPTL mbona unalifinyafinya tu kwa sababu ni jibu ambalo lipo wazi, ripoti ya CAG ipo wazi, ripoti ya kamati ya bunge ipo wazi na juzi mahakama imeamua na siyo kawaida Rais kukaa kimya kwenye mambo kama haya’

Unaweza kuangalia video hii hapa chini

ULIKOSA HII YA ZITTO KUJIBU TAARIFA ZA LIPUMBA KUHAMIA ACT? UNAWEZA KUANGALIA HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments

Advertisement