Siku hizi mbili zimekua na mfululizo wa baadhi ya Wasanii wa Afrika akiwemo Mghana FUSE ODG na Wanigeria Wizkid na Yemi Alade kuonyesha walivyokasirishwa na kituo cha TV cha BET cha Marekani kuwatenga Wasanii wa Afrika na wa Marekani kwa kutoa tuzo za Afrika asubuhi bila shamrashamra huku za kina Beyonce zikitolewa jioni.
Tukiachia hayo ya Afrika, Rapper 50 Cent ambaye amewahi kushinda tuzo nne za BET sasa hivi anazungumziwa sana baada ya kujirekodi akiwatukana waandaaji wa tuzo za BET 2015.
Kilichomkasirisha 50 ni tuzo ya Mwigizaji bora kwenda kwa Terrence Howard ambaye ni staa kutoka kwenye series ya EMPIRE, hii imekua tofauti na matarajio ya 50 ambaye alisema kilichotokea kwenye tuzo za mwaka huu ni aibu.
50 Cent ni kama anaamini mwigizaji Omari Hardwick kutoka kwenye series ya 50 Cent ya POWER ndio alistahili kushinda hiyo tuzo.
Tahadhari, kipisi cha video ya 50 Cent hapa chini kina lugha nzito.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.