Ni Kassim Mapili… mwimbaji mkongwe lakini hata kijana wa sasa hivi atakua amesikia sana moja ya nyimbo zake kubwa za wakati wote…. ina maneno….. ‘napenda nipate lau nafasi…. nipate kusema nawe kidogo rohoni naumiaaaaaa‘
Rais wa shirikisho la Wanamuziki Tanzania Addo November amesema ‘Mzee Mapili hivi karibuni alikua anasumbuliwa na matatizo ya moyo akawa anatibiwa na akapona kabisa na kuendelea na majukumu yake ya kawaida lakini jana aliporudi nyumbani hakutoka tena‘
‘Mzee alikua na vijana watatu lakini hakuwa anakaa nao pamoja na hata mke wake walishaachana, jana alipoingia chumbani kwake hakutoka… majirani walikua wanajua ana tabia ya akiingia kulala anaweza kutoka kesho yake mchana ila leo hakutoka, ikabidi waende Polisi wakaja kuvunja mlango na kukuta alishafariki‘ – Addo November.
https://www.youtube.com/watch?v=BKM4VNk1aD0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE