Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazeti ni hii kwenye gazeti la Jambo Leo yenye kichwa cha habari ‘Jambazi aliyetoroka Mwanza aibua hofu’
#MAJIRA Jambazi aliyetoroka Mwanza aibua hofu, RPC asema lilikuwa tukio la ghafla ikabidi wajihami na mashambulizi pic.twitter.com/GejoQH0MIh
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
Gazeti la Majira limeripoti kuwa baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wamekumbwa na hofu kuhusu usalama wa maisha yao baada ya mmoja kati ya majambazi aliyehusika na mauaji ya waumini watatu katika msikiti wa Rahman na kufanya uhalifu katika maduka ya M-Pesa, Tigo-Pesa, Airtel Money, Hamis Juma (38) kutoroka chini ya ulinzi wa askari Polisi.
Tukio hilo ambalo lilitokea Julai 3 mwaka huu, saa 2:00 usiku katika eneo la mlima Kiloreli Nyasaka, Manispaa ya Ilemela, limeibua hofu kwa wakazi wa jiji hilo kutokana na mfululizo wa matukio ya uhalifu wakidai kushangazwa na jambazi huyo kuwatoroka Polisi.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hilo kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini, walihoji askari wa idara ya upelelezi walijiamini vipi kwenda na jambazi huyo mafichoni kwa wenzake bila kuwa na ulinzi wa kutosha kumfunga pingu za miguu, mikono.
”Tulitilia mashaka tukio hili kutokana na matukio yanayoendelea kutokea, tumezoea kuona polisi wakiwafunga pingu za mikono au miguu watuhumiwa mbalimbali wanaokamata hata kama hana madhara, iweje jambazi asifungwe pingu”
”Jambazi aliyetoroka ameshiriki tukio kubwa la kuuawa watu wasio na hatia, watuhumiwa wa matukio ya kigaidi hupelekwa na mahakamani chini ya ulinzi mkali wa polisi wenye silaha nzito’‘
Akijibu tuhuma hizo, kamanda wa Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi alisema tukio hilo lilikua la ghafla, polisi ni binadamu, wakiwa njiani kwenda mafichoni ghafla majambazi walianza kuwashambulia ikabidi wachukue tahadhari ili kujihami na mashambulizi kwa kujibizana nao risasi ndipo jambazi huyo akatoroka.
Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa zilizoandikwa kwenye magazeti ya July 11 2016
#MWANANCHI India yasaini makubaliano kuisaidia Tanzania ktk sekta ya elimu, afya, maji, viwanda, biashara na kilimo pic.twitter.com/dzjC0dPe7e
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MWANANCHI Mbowe asitisha mpango wa BAVICHA kwenda Dodoma kuzuia mkutano mkuu wa CCM ili kuepusha maafa pic.twitter.com/nxLgkX88Lv
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MWANANCHI RC Iringa, Amina Masenza amekataa madawati 750, adai yametengenezwa chini ya viwango pic.twitter.com/9CYDHZUj0F
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MWANANCHI Uongozi UDART umesema kuanzia mwezi ujao utasitisha matumizi ya tiketi za karatasi na zitatumika kadi pic.twitter.com/UXAREhni5U
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MTANZANIA Watafiti wamegundua kuwa kuwasifu watoto kupita kiasi ni 'mwelekeo usiofaa' pic.twitter.com/xAvsAX54LT
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MAJIRA Miili ya watu tisa waliozama mto Ruvuma ajali ya boti imepatikana na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu pic.twitter.com/vNb8cXvx4C
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MAJIRA India yaipatia Tanzania dola mil 500 kwa ajili miradi ya maendeleo ili kukuza ushirikiano wa kiuchumi pic.twitter.com/ACWkI72Sjt
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#HabariLEO Watumishi wawili kituo cha afya Shinyanga wasimamishwa kazi baada ya mjamzito kujifungulia kwenye varanda pic.twitter.com/ryHyNkYWoF
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MWANANCHI Mtoto wa miaka minne auawa Dar, mwili wakutwa umening'inizwa kisimani, vidole vya mikono vikiwa vimekatwa pic.twitter.com/Ra3hEYZTWr
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MWANANCHI Hospitali ya Rufaa Dom yakabiliwa na upungufu wa wataalamu wa x-ray, ultrasound na kusababisha msongamano pic.twitter.com/QLJjrPozFa
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MWANANCHI Mafuta ya kula Tarime yaadimika, bei yake yapanda, lita 20 iliyokuwa ikiuzwa 45,000 imepanda hadi 56,000 pic.twitter.com/zgoSDRKCNY
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MWANANCHI Kocha mpya Azam, Hernandez asema nyota anayetaka kubaki Azam lazima aonyeshe uwezo, ushirikiano uwanjani pic.twitter.com/zYTbZA9QdG
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MWANANCHI Ureno imetwaa ubingwa wa Euro 2016 baada ya kuwachapa Ufaransa 1-0 pic.twitter.com/6U4Xk0fM4B
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MWANANCHI Kiungo wa Simba, Jonas Mkude amekwenda Afrika Kusini kufanya majaribio ktk klabu ya Mpumalanga Black Aces pic.twitter.com/K4BaNStWVD
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MWANANCHI Mourinho aanza kazi Man United afuta mbinu za Van Gaal, aamuru kuondolewa kamera za uwanja wa mazoezi pic.twitter.com/Ryjgn21RLP
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MTANZANIA JPM ahutubia kwa kiswahili dhifa ya Taifa aliyomwandalia waziri mkuu wa India, asema lengo ni kukitangaza pic.twitter.com/n5GNhoifsR
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
#MTANZANIA Ewura imesema kuna mafuta ya aina zote ya kutosha na hakuna kinachoonyesha kutokea upungufu siku zijazo pic.twitter.com/68cPWnKMV0
— millardayo (@millardayo) July 11, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 11 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI