May 10 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda pamoja na mkuu wa wilaya Kinondoni Ally Hapi kukamata mifuko ya sukari ambayo ilikuwa imefichwa kwenye jengo na mmiliki kusema sukari hiyo sio ya biashara bali ni kwa ajili ya misaada ambapo pamoja na majibu hayo Makonda aliagiza jeshi la Polisi kuendelea kumhoji.
May 11 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ameendelea na zoezi hilo ambapo ametembelea maeneo mawili tofauti na amebaini uwepo wa sukari inayosadikiwa kufichwa kwenye makontena na Godown.
Eneo la kwanza linaloonekana kwenye video fupi hapa chini, RC Makonda amebaini uwepo wa zaidi ya makontena 115 ya sukari iliyofichwa kwenye bandari kavu ya PMP, Makonda ametoa taarifa kuwa kuna zaidi ya Makontena 162 na sio 115 kama ilivyoripotiwa hivyo ameagiza zoezi la ukaguzi wa sukari liendelee kwenye Bandari kavu hiyo.
Eneo la pili ambalo linaonekana kwenye video fupi hapa chini RC Makonda amebaini uwepo wa zaidi ya tani 3000 za mifuko ya sukari elfu ishirini na mbili katika Godown la Mohamed Enterprise ambapo wahusika wamedai sukari hiyo ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani (sukari nyeupe).
RC Makonda ameagiza sukari hiyo isitoke mpaka uchunguzi kutoka TFDA utakampokamilika na ametoa masaa 24 wahakikishe wamepeleka document sahihi zinazoonyesha ni sukari ya viwandani au kingine.
A video posted by millard ayo (@millardayo) on
ULIIKOSA HII YA NAULI ZA MABASI MAPYA YA HARAKA? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE