May 04 2016 Wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo wamekutana na waandishi wa habari na kutoa tamko la kuufungia wimbo wa Snura ‘chura’ kuchezwa kwenye MEDIA kuanzia leo mpaka hapo Snura atakapoifanyia marekebisho video ya wimbo huo na kutoa wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamii.
Sababu za kuufungia ni kinachoonekana ndani ya video ambapo pia Serikali imetangaza kusitisha maonyesho yote ya hadhara ya Snura mpaka atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi zake za sanaa katika baraza la sanaa la taifa BASATA.
Akizungumza Kaimu Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini, Zawadi Msalla amesema……..
>>>’Serikali imesitisha wimbo na video ya chura kupigwa katika vyombo vyote vya habari, maeneo ya wazi na maeneo yote baada ya kuangalia na kuona miondoko iliyotumika katika utengenezaji wa video ile kwanza ni ya udhalilishaji, aina maadili ya mtanzania na ukiukwaji wa haki za binadamu’.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIKOSA ALICHOZUNGUMZA SNURA KUHUSU ISHU YA MAADILI NA KUTOIPELEKA VIDEO YA CHURA KWENYE TV STATION? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI