Leo May 05 2016 Snura Mushi amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia ishu ya wimbo wake wa ‘chura’ kusitishwa, mbele ya waandishi wa Habari Snura amewaomba radhi wananchi kwa kutoa nyimbo ya ‘chura’ ambayo imesitishwa na serikali kwa kuiona nyimbo hiyo ina udhalilishaji na haipo kimaadili ya kitanzania.
Aidha hapo awali serikali ilitangaza kusitisha maonyesho yote ya hadhara ya Snura mpaka atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi zake za sanaa katika baraza la sanaa la taifa BASATA.
Leo Snura ameyazungumza haya.……>>>’Kutoka sasa mimi nimeshajisajili naweza kufanya show hata usiku wa leo kwa hiyo Snura hajafungiwa tena kufanya show zake aliyebaki ni chura ambaye nikifanya video mpya naye chura anakuwa huru kwa hiyo nimeanza kuwa huru mimi kwanza na chura anafuta’
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIKOSA SERIKALI ILIPOTANGAZA KUIFUNGIA VIDEO YA ‘CHURA’ YA SNURA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI