March 23 2016 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatekeleza agizo la kutoa huduma za afya bure kwa wazee wote nchini.
Hii ni baada ya leo kukutana na Baraza la wazee wa Dar es salaam na kusikiliza changamoto zao katika jamii, Waziri Ummy amesema
’Tunataka kuwathibishia wazee wote kuwa ya Serikali ni kuwapatia matibabu bure, kuanzia gharama ya kumuona Daktari, vipimo na Dawa. Pia naziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatekeleza Sera ya Serikali ya kutoa huduma za afya bure ikiwemo kuanzisha dirisha la wazee‘.
’Katika kuonyesha kwamba nimedhamiria, nimeshaongea na watu wa bima ya afya mwezi ujao tutatoa matangazo ambayo tutaweka katika vituo vyote vya Serikali , na tayari tumeshaanza tunatafuta siku ya kuyazindua ili kuendelea kuhamasisha kipaumbele kwa wazee‘
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE
Uliikosa hii Video ya Dyna Nyange kaeleza alivyojibiwa na Alikiba, baada ya kuomba collabo mara mbili?