Tulilijua kwa ukubwa jina la Habida baada ya kutoa hit single ya kesho zaidi ya miaka mitano iliyopita akiwa ni mwimbaji kutokea Kenya.
Kwenye interview na show ya Mambo Mseto ya Radio Citizen Kenya, kwa mara ya kwanza Habida amefungua kinywa chake na kukiri aliwahi kubakwa akiwa mdogo.
Ilitokeajie???? >>>>>> ‘Nilikua bikra wakati huo na huyo Mwanaume alikua akisema wewe nitakupata tu, sasa siku moja ilitokea nikawa nimetoka na marafiki zangu, nikalewa na wakati nataka kwenda nyumbani huyu Mwanaume akasema atanipeleka nyumbani lakini hakunifikisha, ndio akanibaka‘
Kwenye sentensi nyingine, Habida amesema anataka kuwaonyesha Wanawake wengine kwamba hata kama ukibakwa haimaanishi ndio umefeli maisha, anataka kutumia kilichomtokea kuonyesha Wanawake wengine kwamba hata kama kuna kitu kilitokea hakikuharibu maisha yake, yuko hapa na ameendelea na maisha, single yake mpya inaitwa Keep on walking.
Kwa stori zaidi kutoka kwenye makao makuu ya Mambo Mseto unaweza kutembelea msetoea.com