Unaambiwa idadi ya watu walionyongwa imekua na tofauti katika mwaka 2013 na 2014 kwenye nchi mbalimbali duniani ambapo mwaka 2013 watu waliohukumiwa kunyongwa ni 778 kote duniani tofauti na mwaka 2014 ambapo walionyongwa ni 607 imeshuka kwa ongezeko la sawa na asilimia 22.
Sawa idadi ya walionyongwa imeshuka lakini taarifa ikufikie tu kwamba idadi ya waliohukumiwa kunyongwa kwa mwaka 2014 ni 2,466 ni idadi ambayo imepanda kwa asilimia 28 ukilinganisha na mwaka 2013.
Kwenye hii picha hapa chini ndio unapata picha kamili nchi zilizoongoza kwa kunyonga watu mwaka 2014.
Nchi iliyoshika namba 1 ni Iran kwa kunyonga watu 289, ya pili ni Saudi Arabia kwa kunyonga watu 90, ya tatu ni Iraq ambayo ilinyonga watu 61, ya nne ni Marekani iliyonyonga watu 35 na Yemen ndio wamechukua namba 5 kwa kunyonga watu 22.
Nchi ambazo zina idadi ndogo ya watu walionyongwa ni Singapore iliyonyonga watu wawili, Gaza/West Bank watu wawili, Japan watu watatu.
Kwenye nchi za Afrika zilizoongoza kwa kunyonga watu mwaka 2014 ni Sudan 23, Egypt ndio imeshika namba 2 kwa kunyonga watu 15, Somalia 14 wamechukua namba tatu na wa mwisho kwenye hii list Equatorial Guinea walionyonga watu 9.
Ninazo zote kubwa za kila siku na ukijiunga na mimi kwenye facebook bonyeza HAPA Twitter bonyeza HAPA Instagram bonyeza HAPA na unaweza pia kujiandikisha niwe nakutumia kila stori kwenye email sekunde chache tu baada ya stori kunifikia, kuna sehemu ya kujiandikisha upande wa kushoto millardayo.com