Kamishna Mkuu wa Jeshi la polisi Zanzibar, CP Hamad Khamis Hamad amesema hakuna sheria inayowaruhusu Polisi Zanzibar kuwakamata watu wanaokula hadharani mchana wa Ramadhani na kusema chanzo cha msako uliofanyika ni baada ya video iliowaonesha watu wakivuta bangi mchana maeneo ya Maisara Zanzibar.
CP Hamad ametoa ufafanuzi huo kufuatia operesheni iliofanyika Mkoa wa Mjini na kuwakamata Watu waliodaiwa kula mchana wa Ramadhan “Hakuna sheri inayokataza Watu wasile mchana wa Ramadhani, nilitoa maelekezo baada ya video ya wanaovuta bangi kwamba ifanyike oparesheni wale wavuta bangi kwasababu bangi ni kosa la jinai hakuna sheria inayoruhusu Watu kuvuta bangi ila hatukuwakamata wala mchana”
“Shida iliyojitokeza operesheni hii ilikamata waliomo na wasiokuwemo, wavuta bangi na waliokula hadharani, Mampaka nyingine za Kiserikali huwa zinafanya oparesheni hiyo ya wanaokula mchana na wajibu wetu ni kusimamia ili ili zifanyike kwa salama na amani”