Duniani

Unajua maeneo 15 ya India ambako ni MARUFUKU kupiga ‘selfie’? Sababu ni hii..

on

Najua nina watu wangu wao na selfie damdam, taarifa ikufikie kwamba kuna maeneo imebidi selfie zipigwe marufuku kwa ajili tu ya usalama wa watu.

No-Selfie-Zones

Sababu ya Serikali kuamua kuingia kati na kuzuia selfie ni ishu za ajali zinazosababisha vifo, kuna ajali ambazo India wanazo kwenye record zao !! Iko ishu ya ajali ya mtalii mmoja kufariki baada ya kuteleza kwenye ngazi za makumbusho ya Taj Mahal, India alipokuwa akijipiga selfie.

ap564815081655

Iko pia stori ya wasichana wawili walioanguka baharini kutoka kwenye ukuta wa ukingo wa bahari wakijipiga selfie, mmoja akafariki mwingine akatoka salama… Jeshi la Polisi limeona kuna kila sababu wakasogea hatua moja kwa kutangaza maeneo 15 ambayo ni hatari na ni marufuku kupiga selfie..

Sehemu kubwa ya maeneo ambayo ni marufuku kupiga selfie kwa Mumbai India, ni maeneo ambayo yanatembelewa na ni kivutio kikubwa cha watalii wengi.

Kingine ni kwamba kuna mpango wa kuwekwa pia mabango yaliyoandikwa ‘No Selfie Zone

Story ya ajali ya wasichana waliotumbukia kwenye maji wakati wakijipiga selfie.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments