Rapper aliye kwenye orodha ya Mamilionea wa Hiphop duniani 50 Cent alikutana na Interview ya Radio ambapo moja kati ya maswali aliyoulizwa ni kwa nini hakuonekana kwenye pambano la rafiki yake Floyd May Weather April 2015.
50 Cent alikua na haya ya kusema >>> “Sio kwamba sikutaka kwenda.. nilipania kwenda,isitoshe nilipewa ticket nne za lile pambano na HBO, kama mnavyojua niliweka dau juu yake..So nlivyotoka kwenye party nliohudhuria chini ya HBO nkaona nikajiandae niende. Lakini baada ya kuvaa na kila kitu roho ikasita tuu na nikajikuta nimegairi kwenda na nikaona bora kwenda sehemu tofauti kabisa…kusikilizia pambano litaishaje“

‘Nilihisi media itashambilia uwepo wangu tofauti na dhamira ya mimi kwenda … kuhusu dau la millioni 1.6 yes niliweka dau hilo ikiwa tuu atashinda, sikujali angerusha ngumi ngapi au jabs ngapi dau lilikua yeye ashinde pambano achukue pesa, lakini badaae nlikuja kulifuta dau hilo,baada ya mimi na yeye kupatana siku chache kabla ya pambano lake..lakini mwisho wa siku kama mlivyo ona alishinda..!
