Swali lilitoka kwa Mbunge Hamad Rashid Mohammed leo June 25 2015 ndani ya Kikao cha Bunge Dodoma>>> “Wizara hufanya upembuzi katika ujenzi wa barabara zote lakini muda mfupi unakuta barabara zinavimba, Waziri alisema ni kwa sababu ya magari makubwa. Ni sababu ipi inayofanya baada ya muda mfupi barabara zinavimba?”>>>
Majibu ya Waziri Magufuli yako hapa >>> “Si kweli kwamba kila barabara inavimba, kuvimba kwa barabara ni kitu cha kawaida.. Barabara ya kutoka Dar kwenda Mbeya imetengenezwa mwaka 1972, mpaka sasa ni kama miaka 40. Barabara kama hiyo ikiisha muda wa miaka 20 lazima iaanze kuharibika ndio maana ukarabati umeanza kufanyika”>>>
“Ni ukweli kwamba uzidishaji wa magari katika barabara nao inachangia kuharibu barabara, uzito wa magari unaoruhusiwa Tanzania ni tani 56 wakati nchi kama za Ulaya uzito wa juu mwisho ni tani 44, Marekani ni tani 36… Yapo magari huwa yanazidisha mpaka tani 100, tuzingatie Sheria ili barabara zidumu kwa muda mrefu”>>> Waziri wa Ujenzi, John Pombe Magufuli
Hiyo stori iko kwenye hii sauti hapa niliyorekodi Bunge leo June 25 2015