Top Stories

Vurugu nyingine Bungeni July 3 2015 zimefanya hawa Wabunge wapigwe STOP kuingia bungeni. (Audio)

on

32July 3 2015 imekuwa siku nyingine ambayo kikao cha bunge Dodoma hakijaisha kwa amani, Wabunge wa Upinzani kwa mara nyingine walipinga Bunge kuendelea kujadili miswada ambayo iliwasilishwa.

Baada ya Kikao cha Bunge kuahirishwa asubuhi, Jioni Kikao kiliendelea tena ambapo kwanza ilisomwa taarifa kuhusu ishu ya utata uliotokea Bungeni kuwasilishwa kwenye Kamati ya Maadili na yakatolewa maamuzi ya Kamati hiyo.” hayo maneno ameyasema Mwenyekiti wa Kamati, Hassan Ngwilizi

IMG_1457Vitendo vilivyofanywa na Wabunge hao ni ukiukaji wa Kanuni za Bunge… Kamati imeamua Wabunge Tundu Lissu, John Mnyika, Moses Machali, Pauline Gekuu na Felix Mkosamali wasihudhurie vikao vyote vilivyosalia kwenye mkutano wa 20 kuanzia tarehe 4 Julai 2015” – Hassan Ngwilizi.

IMG_1460

Kamati pia imeamua wabunge Rajabu Mbarouk na Mchungaji Peter Msigwa wasihudhurie vikao viwili vya mkutano wa Bunge kuanzia tarehe 4 Julai 2015, na Wabunge Joseph Selasini, Khalifa Suleiman Khalifa na Rashid Ali Abdallah wanatakiwa kufika mbele ya kamati ya maadili Jumamosi saa nne asubuhi kwa kuwa hawakupata hati ya kuitwa kwa haraka.” >>> Mwenyekiti wa kamati ya haki, kinga na maadili ya Bunge, Brigedia Mstaafu Hassan Ngwilizi.

Spika wa Bunge akaahirisha Kikao baada ya maamuzi hayo ambapo sauti zote za hili tukio ziko hapa chini mtu wangu, ukiplay utasikiliza kilichotokea Bunge.

Hapa anasikika Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Hassan Ngiwilizi akisoma Maazimio ya Bunge.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments