Top Stories

Hizi ndio sababu zilizofanya Saed Kubenea agombee Ubunge, na ajiunge CHADEMA… (Audio & Pichaz)

on

DSCI0119

July 21 2015 siku imebebwa na headlines nyingine za Siasa, jina la Saed Kubenea linafahamika na watu wengi kwa sababu yeye ni mmoja ya Wanahabari wakubwa sana Tanzania, lakini leo kaamua kuingia kwenye Ulimwengu mwingine tofauti.. YES, ni kutoka kwenye Uandishi wa Habari na kuwa Mwanasiasa, na anaianza safari hiyo kwa kuusaka Ubunge kabisa !!

DSCI0116

Naitwa Saed Kubenea nimeamua Kugombea Ubunge wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA… Nimesukumwa na kauli ya Mwalimu kwamba  Watanzania wanahitaji mabadiliko na mabadiliko hayo yamekosekana kwenye Chama cha Mwalimu sasa ni wakati wa kuyatafuta upande mwingine” >>>> Saed Kubenea.

DSCI0127

Wapo waliomsindikiza pia kutangaza kugombea Ubunge.

Unajua kilichofanya agombee Ubunge? >>>> “Nahitaji kusaidia taifa langu kuwa miongoni mwa watunga Sheria na wasimamizi wa Serikali…. Nimefanya kazi hii kupitia kalamu kama Mwandishi wa Habari lakini mmeona jinsi ambavyo Serikali kukandamiza uhuru wa Vyombo vya Habari, badala ya kutumia kalamu sasa niingie Bungeni nisaidie upatikanaji wa haki ya msingi ya raia kupata habari… niwe sehemu ya Bunge ili kuwawakilisha Watanzania kuhakikisha nchi inapata Sheria bora na safi  za Uhuru wa habari” >>>> Saed Kubenea.

DSCI0114

Saed Kubenea.

Hizi ndio sababu alizozitaja kuamua kugombea Ubungo Dar >>>> “Siwezi kwenda kwenye Chama ambacho najua hilo Jimbo hakitapewa, nimeenda kwenye Chama ambacho najua hilo Jimbo kitakabidhiwa ndio maana nimeenda CHADEMA… Siamini kama mimi na Mnyika tukaingia kwenye msuguano lakini akiamua Kugombea Jimbo la Ubungo nitamwachia, lakini naamini na ninamshauri kwamba Mnyika ameshafanya kazi kubwa Jimbo la Ubungo aende Kibamba, atuachie hawa wezi wa Ubungo tushughulike nao sisi” >>>> Saed Kubenea.

DSCI0120

Iko hapa sauti ya Saed Kubenea akiwa anatangaza kugombea Ubunge.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments