Ni zaidi ya miezi saba imepita toka Bunge litoe mapendekezo kwamba wahusika wote wa ishu ya ESCROW wawajibishwe, kazi ikaanza kwenye Kamati ya Maadili ambapo Viongozi mbalimbali walianza kuhojiwa ikiwemo Mbunge Anna Tibaijuka, Andrew Chenge na William Ngeleja.
Kwa upande wa Andrew Chenge Kamati hiyo ilisimamisha kumhoji kwa vile alikuwa amepeleka ombi Mahakama Kuu kuzuia kuhojiwa, baadae Mahakama hiyo ikatoa amri kwamba Kamati ya Maadili inaweza kuendelea na kumhoji.
July 27 2015 ilikuwa Mbunge huyo afike kwenye Kikao cha Kamati ya Maadili Dar kwa ajili ya kuhojiwa na kuhusika kwake kwenye ishu ya ESCROW, lakini ripota wa millardayo.com kafika kwenye Ofisi za Kamati hiyo.
Mbunge huyo hakufika na taarifa iliyotolewa ni kwamba Andrew Chenge ameomba Kamati ya Maadili ipeleke mbele tarehe ya kusikiliza shauri lake kwa vile ratiba hiyo inaingiliana na majukumu yake ambayo CCM imemkabidhi Jimboni kwake Bariadi Magharibi wakati huu wa maandalizi ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015.
#NEWS: Mbunge Andrew CHENGE ameomba Kamati ya Maadili isimamishe kusikiliza shauri lake kuhusu ESCROW kutokana na shughuli za Uchaguzi CCM.
— millard ayo (@millardayo) July 27, 2015
Kwa chochote kinachonifikia kuhusu nitahakikisha unakipata pia mtu wa nguvu.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.