Wenye magari Tanzania leo wana sababu ya kutabasamu maana Kampuni ya magari ya General Motors East Africa (GMEA) Limited leo wamesaini makubaliano ya kibiashara na Quality automotive mechanization limited (QAML) ambayo itashuhudia kampuni ya magari ikiingia kwenye soko la Tanzania.
Kupitia uuzaji mpya, wateja wa General Motors wataweza kununua bidhaa mpya aina ya Isuzu na Chevrolet kutoka katika sehemu za mauzo huku wakipata huduma za kimataifa kutoka katika eneo maalumu la magari hayo.
Akizungumza hi leo wakati wa sherehe ya kutia saini makubaliano ya biashara, Mwenyekiti Mheshimiwa wa QAML Mwenyekiti Mheshimiwa Yusuf Manji aliahidi wateja ngazi bora ya urahisi na faraja, “Tumeweka uwekezaji mkubwa/muhimu kuhakikisha mafanikio ya kituo hiki na kuwezesha kupenya kwa haraka kwa bidhaa za Isuzu na Chevrolet katika soko hili lenye ushindani mkubwa” alisema.
Eneo la mauzo ya magari limetengenezwa ili kutoa/ kuwapatia wateja uzoefu na uimara kwa ujumla na bidhaa za General Motors, pamoja na kutoa huduma za mauzo na vifaa vya magari, Mkurugenzi mtendaji wa GMEA Rita Kavashe alisema Kampuni ya General motors kuingia katika soko la Tanzania ilikuwa ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu katika kampuni hiyo ili kuimarisha uwepo wake katika Afrika Mashariki.
“Tanzania imejitokeza katika soko na kama General Motors tulitaka kuwa sehemu ya ukuaji huu. Sehemu hii ya mauzo itakuwa ni hatua ya kuingia kwa bidhaa zetu zenye ubora na zimetumia utaalamu mkubwa katika utengenezwaji wake ambapo tunatanua wigo wetu katika ukanda huu. Kupitia uuzaji huu, wateja wetu watanunua aina mpya za Chevrolet na Isuzu huku wakipata huduma bora”.Alisema
Bi. Kavashe alisema kuingia ndani ya soko la Tanzania imetokana na kukua kwa kasi kwa biashara ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki hasa katika kuendeleza ushirikiano wa masoko ya umoja. Soko la jumuia ya Afrika Mashariki lina takribani watu milioni 140.
“Tanzania ni soko linalokua kwa kiwango kikubwa na imekua ni soko muhimu tunalolitazamia tunapotafuta kujikita katika soko lenye watu wengi na idadi inayokua kila kukicha. Ukuaji wa viwanda na kuongezeka kwa kipato ili kutengeneza ongezeko la watu wa tabaka la kati katika nchi hii ina maana kuwa kuna soko changa la bidhaa zetu, “aliongezea Kavashe.
General Motors Co. (NYSE:GM, TSX: GMM) na washirika wake wanatengeneza magari katika nchi 30, na kampuni ina nafasi za uongozi katika masoko makubwa ya magari na yanayokua haraka duniani. GM, tanzu zake na vyombo vyake vya ubia wanauza magari chini ya bidhaa za Chevrolet, Cadillac, Baojun, Buick, GMC, Holden, Jiefang, Opel, Vauxhall na Wuling. Taarifa Zaidi kuhusu kampuni na tanzu zake zikiwemo On Star, kampuni inayoongoza duniani katika usalama wa magari, huduma na taarifa za usalama, zinapatikana http://www.gm.com
General Motors East Africa Limited (GMEA) Ilianzishwa 1975 kama muungano kati ya serikali ya kenya na kampuni ya General Motors. GMEA ilianza kutengeneza magari mwaka 1977 na ni kiwanda kikubwa cha magari ya biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kiwanda chake cha Nairobi kinatengeneza magari makubwa aina ya Isuzu na mabasi, na wanauza magari yaliyotengenezwa kikamilifu aina ya Chevrolet kwa ajili ya abiria. Kuanzia kampuni ilivyoanzishwa imetengeneza Zaidi ya vitengo 70,000.
GMEA imekua ikiongoza sokoni nchini kenya kwa miaka 3 tangu mwaka 2012. Mwaka 2014 ilikuza hisa zake sokoni na kufikia 28.7% – ushahidi tunao kwa bidhaa zake imara na huduma bora kwa wateja. Kutokana na vyanzo vizuri vya fedha na vya kiteknolojia , GMEA imekua ikijulikana Zaidi na kuunganisha Zaidi wauzaji (mauzo, mgawanyo, na huduma) katika miji mikubwa Afrika Mashariki.