Hawa ndio wakali wengine watano Ligi ya Uingereza wenye utajiri mkubwa zaidi, na pichaz zao…
Share
3 Min Read
SHARE
Mastaa wa soka wana utajiri wao wa kutosha tu, unaambiwa kutokana na kazi nzuri wanayoifanya hata thamani yao inaongezeka vilevile, ukisikia staa wa soka kanunuliwa kwa pound. Mil 100 Uingereza basi uwe na jibu kabisa kwamba YES jamaa ni jembe la kazi !!
Lakini thamani yake haiishii uwanjani, hata nje ya Uwanja jamaa wa Kampuni kama Nike, PUMA, ADIDAS hawamwachii apite hivihivi wasimpe hata dili moja eti?
Soka na maisha yao nje ya Uwanja vinasababisha wajikusanyie pesa na wawe na utajiri wa kutosha kabisa… karibu uipitie hawa watano ambao wametajwa kuwa na utajiri wa juu zaidi kwenye List ya mastaa wanaochezea Ligi Kuu Uingereza!!
No.5:Utajiri wake unakadiriwa kuwa kama Dola Milioni 55, umri wake ni miaka 27 tu lakini tayari kaonesha Ulimwengu jinsi ambavyo ana uwezo mkubwa Uwanjani kitu ambacho kimempa thamani ya juu pia kati ya mastaa wa Uingereza… Jamaa anachezea Klabu yaManchester City.No.4: Bastian Schweinsteiger, moja ya Vifaa vya nguvu ambavyo vimeenguliwa kutoka Bayern Munich msimu huu na kujiunga na Man United.. Kama akionesha uwezo zaidi basi huenda akapanda chati na kuuongeza utajiri wake ambao kwa sasa ni kama Dola Mil. 60 hivi.No.3:Japo umri wake ni mkubwa, miaka 34 lakini hata akisema anastaafu leo Klabu ya Chelsea itakuwa na heshima kubwa kwake kwa mchango mkubwa alioutoa kwa Klabu hiyo kwa miaka mingi ambayo ametumia akiichezea Klabu hiyo. Yuko vizuri pia kwenye nafasi ya tatu akiwa na utajiri waDola Mil. 65.No.2: Yaya Toureni nafasi ya pili na ndio staa wa Soka pekeake kwenye hii list ya watano ambae ana asili ya Afrika. Utajiri wake ni kamaDola Mil. 75.. Jamaa ni mmoja wa vichwa ambavyo vinategemewa sana Man City.No.1: Mkali wa Uingereza na mwenyeji wa hapohapo yani.. Kichwa kinachofanya vizuriManchester United, na ni mmoja ya wakali ambao Uingereza na Man United wanajivunia sana, ukali wake umefanya akae #1 na utajiri wake ni Dola Mil. 110 akimuacha Yaya kwa Dola Mil. 35 hivi !!
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> TwitterInstaFBna nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa>>>Videosili kila video ya AyoTV ikufikie.