Timu ya taifa ya Brazil imekumbana na wakati mgumu katika mchezo wa Copa America 2016 dhidi ya Peru uliochezwa alfajiri ya June 13 2016, mchezo huo wa Kundi B ulikuwa unawapa nafasi kubwa Brazil kuibuka na ushindi, hususani takwimu ya kumiliki mpira kwa asilimia 66 ili wafanya Peru wacheze kwa kulinda goli zaidi.
Licha ya kuwa Brazil kuwa nafasi ya 7 katika viwango vya FIFA na Peru nafasi ya 48, walikubali kuruhusu goli dakika ya 75 baada ya Raul Ruidiaz kufanikiwa kufunga goli linaloaminika kuwa la mkono kwa wachezaji wa Brazil, goli hilo lilifanya mchezo kusimama na muamuzi kuvuta muda wa kufanya maamuzi.
Ujanja wa Raul Ruidiaz umeisaidia Peru kutinga hatua inayofuata na kuifanya Brazil kufungasha virago na kurejea Brazil, baada ya mchezo huo Brazil wamesalia na point 4 wakiwa nafasi ya tatu nyuma ya Ecuador na Peru anayeongoza kwa jumla ya point saba.
#MillardAyoUPDATES #LiveMatch #FullTime #Brazil 0-1 #Peru (#Ruidiaz 75′) #CopaAmerica #Brazil wametolewa rasmi pic.twitter.com/5TcdDBx267
— millard ayo (@millardayo) June 13, 2016
ALL GOALS: TAIFA STARS VS MISRI JUNE 4 2016, FULL TIME 0-2
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE