Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michael Platini leo May 9 2016 ameingia kwenye headlines, baada ya majibu ya rufaa yake ya kufungiwa miaka sita kujihusisha na soka kukataliwa kufutwa na badala yake amefanikiwa kupunguza kifungo hicho kutoka miaka sita hadi miaka minne.
Baada ya kukataliwa kufutwa kwa kifungo chake Michael Platini ametangaza kuwa atajiuzulu nafasi yake katika bodi ya uongozi wa soka barani Ulaya, Mahakama ya michezo (Court of Arbitration for Sport (Cas) ili amua kumpunguzia adhabu Jumatatu ya May 9 2016 na kumfungia kwa miaka minne.
Platini ambaye ana umri wa miaka 60 alifungiwa miaka sita kutojihusisha na soka kutokana na kukubali au kuhusika kupokea malipo ya pound milioni 1.3 mwaka 2011 kutoka kwa aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter, malipo hayo yanatajwa kuwa hayakuwa halali na yanatajwa kuwa yalitumika kumfanyia kampeni Blatter.
GOAL: SIMBA VS MWADUI FC MAY 8 2016, FULL TIME 0-1
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE