April 27 2016 nusu fainali ya pili ya michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya iliendelea, baada ya Jumanne ya April 26 kushuhudia mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Klabu Bingwa Ulaya iliyokuwa inazihusisha timu za Man City dhidi ya Real Madrid na mchezo kumalizika kwa sare ya 0-0.
Jumatano ya April 27 katika uwanja wa Atletico Madrid unaojulikana kwa jina la Calderon, ulipigwa mchezo wa pili uliokutanisha wenyeji wa uwanja huo dhidi ya FC Bayern, hadi dakika 90 zinamalizika Atletico Madrid walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa dakika ya 11 na Niguez Esclape.
Licha ya kuwa Atletico Madrid wameibuka na ushindi huo, FC Bayern walikuwa wanamiliki mpira kwa asilimia 70 na wenyeji wao asilimia 30, kitu ambacho kitawapa tabu mchezo wa marudiano, Atletico watapata shida na ukilinganisha na rekodi ya FC Bayern ya kupenda kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa.
Video ya magoli ya Atletico Madrid 1 – 0 Bayern Munich
https://youtu.be/QW4jBtmagOI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ALL GOALS: Yanga vs Al Ahly (Full Time 1-1) April 9 2016 CAF
https://youtu.be/VSM0_i0-DY0