Baada ya kutokea kwa tukio la basi lenye kikosi cha Man United kushambuliwa May 10 2016 kabla ya mchezo dhidi ya West Ham United, mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa Boleyn basi la timu ya Man United lilishambuliwa kwa kurushiwa chupa na vitu mbalimbali.
Leo May 14 2016 taarifa za kijana mwenye umri wa miaka 28 kukamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo zimesambaa mitandaoni, kijana huyo ambaye ameshukiwa kuhusika na tukio hilo amefikishwa kituo cha polisi cha East London,
Hata hivyo kabla ya kukamatwa mtu huyo leo May 14, tayari kulikuwa na watu watatu wenye umri wa miaka 18, 20 na 47 wamekamatwa wakihusishwa na tukio hilo lililofanyika May 10 2016, kikosi cha Man United kilishambuliwa kikiwa ndani ya basi muda mchache kabla ya kushuka.
KASEJA KAZUNGUMZIA GOLI ALILOFUNGWA NA TAMBWE MAY 10 2016
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE