Baada ya usiku wa Alhamisi ya March 9 2017 mtanzania Mbwana Samatta kuingia uwanjani na timu yake ya KRC Genk kucheza mchezo wao wa kwanza wa Europa League hatua ya 16 bora dhidi ya KAA Gent na kufanikiwa kufunga magoli mawili katika ushindi wa goli 5-2.
Leo March 12 2017 staa huyo wakiwa ugenini na timu yake ya KRC Genk walicheza mchezo wao wa 30 wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya KVC Westerlo katika uwanja wa Het Kuipje, katika game hiyo Genk walifanikiwa kupata ushindi wa goli 4-o Mbwana Samatta akifunga goli la kwanza dakika ya 7.
Magoli mengine ya KRC Genk yalifungwa na Thomas Buffel dakika ya 27, Omar Colley dakika ya 62 na Malinovsky dakika ya 90 ushindi huo sasa unaifanya KRC Genk kutimiza point 48 katika msimamo wa Ligi, ikiwa imecheza michezo 30, imeshinda michezo 14, sare michezo 6 na imepoteza michezo 10.
Ushindi wa leo unamfanya Samatta ndani ya mwezi March kuwa na rekodi ya kufunga jumla ya magoli matano katika kila mechi aliyoichezea ndani ya mwezi March na ikiwa ni kwa mara ya tatu mfululizo anafunga, alifunga goli 2 za ushindi wa Genk wa goli 2-1 dhidi ya Club Brugge March 4 2017.
EXCLUSIVE: Mishahara ya kwanza ya mastaa wa soka Samatta, Msuva, Maguli, Himid Mao na Bossou