May 17 2016 headlines mpya ambazo imezifikia millardayo.com ni kuhusu sukari, baada ya kuwepo na headlines nyingi kuhusu baadhi ya wafanyabiashara kutuhumiwa na wengine kukamatwa kutokana na kosa la kuficha sukari, habari mpya ni kuwa wafanyakazi wa kiwanda cha sukari Morogoro wamepanga kugoma kuendelea na uzalishaji.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Sukari Ilovo wilaya Kilosa na Kilombero wametishia kusitisha kuendelea na uzalishaji wa sukari, lengo likiwa ni kushinikiza waongezwe mshahara kwa asilimia 15 badala ya asilimia 2.2 aliyokubali kuongeza muajiri baada ya kuvutana kwa muda mrefu.
Mpango wa wafanyakazi hao umeafikiwa baada ya kukaa kikao na mwenyekiti wa wafanyakazi mashambani TPAWU Isaack Magassa na kushauriana kutokana na muajiri kuongeza mshahara kwa asilimia 2.2 tofauti na sheria ambayo inaruhusu ongezeko la mshahara kufikia hadi asilimia 25.
ULIKOSA UJUMBE WA ZITTO KABWE KWA WAZIRI NAPE? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE