May 7 2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans ambao mashabiki wao tayari mtaani wanajitamba na kujiita Mabingwa watarajiwa wa Ligi Kuu, walishuka uwanja wa Taifa kuwakabili wapinazani wao GD Esperanca katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika.
Yanga ambao walipangwa na GD Esperanca baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri jumla ya goli 3-2 katika michuano ya klabu Bingwa barani Afrika, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya wpinzania wao kutokea Angola klabu ya GD Esperanca, lakini Yanga watalazimika kwenda Angola wiki mbili zijazo kucheza mchezo wa marudiano.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kigumu kwa pande zote na kwenda mapumziko bila kufungana, lakini awali Eperanca walikuwa wanacheza mpira wa taratibu na kujitahidi kumiliki mpira ili kuituliza presha ya mchezo, hali ambayo ilifanya Yanga wabadilike na kufanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya 71 kupitia kwa Simon Msuva, kuingia kwa Matheo Anthony kulizaa matunda baada ya dakika ya 90 kufunga goli la pili.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ALL GOALS: Yanga vs Al Ahly (Full Time 1-1) April 9 2016 CAF
https://youtu.be/VSM0_i0-DY0