Rais Barack Obama wa Marekani amekutana na vijana mbalimbali kutoka bara la Afrika ikiwa ni mpango wa serikali yake kila mwaka toka mwaka 2014 kukutana na vijana hao wanaohusika na kuivusha jamii kwenye ishu mbalimbali ikiwemo biashara na siasa.
Mwanaharakati wa haki za binadamu Mtanzania Mwanasheria Geline Fuko kutokea kwa Hellen Kijobisimba kwenye kituo cha sheria na haki na bianadamu ni miongoni mwa vijana takribani 40 kutoka Tanzania ambao walishinda nafasi za kuja Marekani kwenye huo mpango wa Obama.
Geline amevichukua vicha vya habari na kufanya Interview ambazo hata hakutarajia pamoja na kuitwa na watu mbalimbali wakubwa baada tu ya kutajwa na kupongezwa na Rais Obama mbele ya umati mjini Washington DC August 3 2015.
Yafuatayo ni mambo 7 unatakiwa kujua baada ya Geline kutajwa na Obama.
- Rais Obama ana programu inaitwa Mandela Washington Fellowship ambayo kila mwaka kuanzia mwaka 2014 imekua ikiwaleta Marekani vijana kutokea Afrika na kuwapa mafunzo.
- Vijana walio-apply kushiriki kwenye programu hii mwaka huu ni zaidi ya elfu 40 lakini wamechaguliwa elfu moja tu akiwemo Geline Fuko kutoka Tanzania.
- Sio kila anae-apply anaweza kuchukuliwa, moja ya masharti ni kwamba ni lazima kama kijana uwe tayari ulishafanya chochote cha kuisaidia jamii na umri wao ni miaka 25-35
- Rais Obama amempongeza Geline kutokana na juhudi zake za kuwawezesha Watanzania kuweza kuisoma katiba kupitia mtandao kufika mpaka kwenye simu zao za mkononi.
- Kwenye kundi la kina Geline wamesifiwa vijana watatu tu, mmoja ndio yeye kutoka Tanzania na wengine wawili kutoka Afrika Magharibi.
- Vijana hao kutoka Afrika wamegawanyika kwenye makundi mbalimbali ambapo Geline alikua kwenye kundi la mambo ya uongozi na siasa.
- Geline na wenzake wamegharamiwa kila kitu na serikali ya Marekani mpaka kuletwa kwenye mji wa Washington na pia kwa kipindi cha wiki sita walizokaa, wameingia darasani na kufundishwa chuoni na Maprofesa kuhusu maswala ya uongozi kwenye vyuo vikuu.
Unaweza kutazama hapa chini kipisi tu cha video Rais Obama akimsifia Geline Fuko mbele ya vijana wengine wa Afrika pamoja na wahudhuriaji wengine na Interview ya Geline na Millard Ayo itasikika kwenye AMPLIFAYA CloudsFM saa moja usiku leo.
ULIKOSA KUONA SHOW YA DIAMOND ILIYOVUNJA REKODI LAS VEGAS MAREKANI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI…