Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF leo July 12 2016 limetangaza good news kwa mashabiki wa soka ambao huenda huwa wanakosa muda wa kwenda uwanjani kuangalia mechi, TFF leo imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitano na Azam TV kwa ajili ya kuendelea kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara.
Mkataba huu wa Azam TV sasa klabu itakuwa inapewa milioni 126 kwa awamu tatu tofauti na awali ilivyokuwa milioni 100, awamu ya kwanza na pili zitatolewa milioni 42, halafu awamu ya mwisho klabu inayomaliza nafasi za juu zaidi inalipwa zaidi kuliko iliyopo nafasi ya chini, hii inatokana na TFF na Azam TV kuamua kuleta ushindani.
TFF imeingia mkataba wa miaka mitano na Azam TV wa urushaji wa matangazo ya Ligi Kuu, unathamani ya Tsh Bilioni 23 pic.twitter.com/ixcqLvBzfO
— millard ayo (@millardayo) July 12, 2016
GOLI LA MECHI YA YANGA VS TP MAZEMBE JUNE 28 2016, FULL TIME 0-1