Aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alikutana na Wanahabari na kutangaza kuzirejesha Serikalini Tsh. 40.4m alizopewa na James Rugemalira huku akizitaja sababu 5 zilizomfanya aamue hivyo.
Mbunge wa Kawe Halima Mdee yupo nje kwa dhamana baada ya kukaa mahamusu kwa siku 5…hizo ni miongoni mwa stori kubwa zilizopewa nafasi kwenye Magazeti ya Tanzania leo July 11, 2017…zipitie hapa millardayo.com.
Mkutano Mkuu wa BAKWATA Wilayani Maswa umewafukuza viongozi wote wa Baraza hilo kwa ubadhirifu wa Tsh.49.8m za mapato mbalimbali. #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Serikali imewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashuri kuwa makini kwa kuwa sasa inafuatilia nyendo zao ktk utendaji wao #MTANZANIA
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
"Sitaki Watanzania wa maisha ya chini waonewe katika kipindi changu." – Rais JPM. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Imeelezwa kuwa jumla ya ajali 50 zilizotokea Wilayani Kahama kipindi cha January mosi hadi June 30 zimesababisha vifo vya watu 39. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Chama cha Washereheshaji (SAA) kimekubali maelekzo ya Serikali kuwataka Washereheshaji kuingizwa ktk mfumo rasmi wa ulipaji kodi. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Mahakama ya Wilaya ya Chato, Geita imewanyima dhamana viongozi na wafuasi 51 wa CHADEMA baada ya upande wa mashtaka kuomba izuiwe. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Watumishi wenye elimu ya Darasa la 7 wametakiwa kuwasilisha Serikalini vyeti vyao vya kujiendeleza hadi Form 4 vinginevyo watafutwa #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Polisi Tabora kitengo cha Usalama Barabarani imepata pigo baada ya askari wake Koplo Aswile kugongwa na lori na kufariki jana. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Kilimanjaro Veggies Ltd (KVL) inayomilikiwa na Mbowe imemfikisha Mahakamani DC wa Hai ikimdai fidia ya zaidi ya Tsh. 549m. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Mkazi wa Lyapona, Sumbawanga Victoria Landani (67) ameuawa kwa fimbo na marungu na watu 3 akidaiwa kuiba mahindi shambani. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Mbunge Halima Mdee amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais JPM. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itaanza kusikiliza kesi ya shambulio inayomkabili Naibu Waziri wa Fedha wa zamani Adam Malima #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Wakazi wa Mpanda, Katavi wamepewa miezi 6 kuondoka katika maeneo ya hifadhi ya reli kupisha maboresho yanayofanywa na TRL. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya DSM limewakamata watuhumiwa wanane wa wizi wa magari katika eneo la Kongowe mkoani Pwani. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Vyama vinavyounda UKAWA vimeanzisha mkakati wa kumng'oa ktk Ofisi za CUF, Mwenyekiti anayetabuliwa na Msajili Prof. Lipumba. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, DSM August 1 mwaka huu, itaanza kusikiliza kesi ya kada wa CHADEMA, Wema Sepetu na wenzake. #TanzaniaDAIMA
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Mkazi wa kijiji cha Ruaruke, Kibiti, ameuawa kwa risasi na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia jana na mwingine kujeruhiwa. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Wananchi wa Mahiga, kijiji cha Mwakitolyo, Shinyanga wamemuomba Rais JPM amtumbue RC Zainab Telack wakidai anatumia madaraka vibaya. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Wachenjuaji wa dhahabu ktk mgodi wa Mwakitolyo, Shinyanga wamekubaliana kuchangia Tsh.100,000 kila mmoja kwa ajili ya ujenzi wa vyoo. #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Serikali imeombwa kuwasamehe kodi wafadhili mbalimbali wanaokuja nchini kwa lengo la kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji maalumu. #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
BAKWATA imetaka Watanzania watulie ikifanyia uchunguzi taarifa inayosambaa kuwepo mtu anayedai kuoteshwa na kufanana na Mtume El-yasa #UHURU
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
CCM Kilimanjaro imepata ushindi katika uchaguzi mdogo wa marudio ya Serikali za mitaa katika vijiji vinne, vitongoji 19, wajumbe 53. UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngeleja amezitaja sababu 5 za kurejesha Tsh. milioni 40.4 alizopewa na Rugemalira. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
M/kiti wa Jumuiya ya Wazazi, Abdalla Bulembo amemshauri Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif kuachana na siasa na kulinda heshima yake. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 11, 2017
“Sasa hivi tumeweka sheria mpaka majipu yanajitumbua yenyewe” – JPM
GUMZO LA ESCROW: Sababu 5 za William Ngeleja kurudisha Fedha za ESCROW!!!