Mix

PICHA 3: Watu walivyolala nje ya nyumba Bukoba kwa kuhofia tetemeko usiku

on

September 10 2016 lilitokea tetemeko la ardhi Kagera kanda ya ziwa Tanzania lenye kipimo cha 5.7 na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa ambapo ndani ya saa 24 baadae (September 11 saa tano kasoro usiku) likatokea tena tetemeko jingine.

Tetemeko hilo la pili ambalo ni dogo halijaripotiwa kusababisha majeruhi au vifo mpaka usiku wa saa nane lakini limeleta hofu kwa wakazi wa Bukoba ambao baadhi wameamua kutoa magodoro nje ya nyumba zao na kulala kwa kuhofia tetemeko linaweza kutokea tena na kuwakuta ndani ya nyumba zao.

screen-shot-2016-09-12-at-2-23-25-am

screen-shot-2016-09-12-at-2-20-58-am

millardayo.com na AyoTV zinaendelea kufatilia kwa ukaribu kila taarifa na zitakufikia kila wakati zinapotoka ila kwa sasa unaweza kusikiliza kwa kubonyeza play hapa chini kuipata ripoti ya kwanza ya Mwandishi wa habari baada ya tetemeko la pili kutokea Bukoba.

ULIIKOSA RIPOTI YA KWANZA YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA BAADA YA TETEMEKO LA KWANZA BUKOBA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments