Moja kati ya habari zinazo-trend katika soka leo October 9 2016 ni kuhusiana na list ya wachezaji bora wa muda wote wa LaLiga, kituo cha uchunguzi, histoaria na takwimu za soka Hispania (CIHEFE) kimetaja majina ya wachezaji bora wa muda wote katika historia ya LaLiga.
Licha ya kuwa utafiti huo wa CIHEFE uliotaja list hiyo kuanza kuleta minong’ono katika mitandao, wengi wameshangazwa kuona mshindi wa tuzo tatu za Ballon d’Or Cristiano Ronaldo kuwekwa namba 23 na mpinzani wake wa karibu katika soka Lionel Messi wa FC Barcelona kupewa nafasi ya nne.
Namba moja ya list hiyo amepewa Raul Gonzalez mkongwe wa zamani wa Real Madrid, mkongwe Cesar Rodriguez yupo namba 2, Telmo Zarra namba tatu, Lionel Messi nafasi ya nne na Enrique Castro ‘Quini’ nafasi ya tano, wachezaji kama David Villa yupo nafasi ya 32, Xavi nafasi ya 49 wakati Iker Casillas ameshika nafasi ya 62.
Imetajwa List ya wachezaji bora wa Laliga wa muda wote, Raul namba 1, Messi namba 4 wakati Cristiano Ronaldo yupo namba 23 #CIHEFE pic.twitter.com/GEOSGWO7Ha
— millard ayo (@millardayo) October 9, 2016
ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1