Ikiwa ni siku 11 toka Mwigizaji Mzee Majuto afariki, leo August 19, 2018 Mke wake ambae walizaa watoto wanne pamoja akiwa ameambatana na Mdogo wa mwisho wa Mzee Majuto, wameibuka kwenye Vyombo vya Habari na kudai kuwa Watoto wa marehemu pamoja na Ndugu wa Mzee Majuto ‘wamemfukuza’ Tanga.
Kwa upande wa pili, Mohamed Amri ambae ni Mtoto Mkubwa wa Mzee Majuto wa pili kuzaliwa amesema sio kweli kwamba Bi. Aisha amefukuzwa Tanga na kwamba walimuuliza angependelea eda yake aifanye Tanga au Dar kwa Baba mzazi kisha yeye akachagua kwa Baba yake Mzazi.
Mohamed amesema Tanga ni nyumbani kwake (Aisha) na wala hajafukuzwa kama alivyoongea na vyombo vya habari hivyo mlango uko wazi akitaka kurudi.
INTERVIEW YA MWISHO YA MZEE MAJUTO: “HUYU NDIO ATAKUA MRITHI WANGU”
MSIKITI ALIOJENGA MZEE MAJUTO NA NYUMBA ANAZOMILIKI… BONYEZA PLAY KUTAZAMA HAPA CHINI