Michezo

Rekodi ya Jose Mourinho vs Arsene Wenger kabla ya kukutana Nov 19 2016

on

Moja kati ya michezo ya soka itakayovuta hisia za watu wengi ni mchezo kati ya Man United dhidi ya Arsenal utakaochezwa Jumamosi ya November 19 2016 katika uwanja wa Old Trafford, huu ni mchezo unaomkutanisha Jose Mourinho na Arsene Wenger.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger na kocha wa Man United Jose Mourinho Jumamosi watakuwa wanakutana kwa mara ya kumi na sita, Jose Mourinho akiwa na vilabu viwili tofauti alikuwa na Chelsea na sasa anaifundisha Man United.

screen-shot-2016-11-17-at-6-48-23-pm

Mourinho amecheza na Arsenal ya Wenger mara 15 akiwa kafanikiwa kumfunga mara nane na kukubali kufungwa mara moja huku mara sita wakiishia kutoka sare, Wenger wamefungana na Mourinho mara 1 katika mchezo wa Ngao ya hisani, huku Wenger akifungwa mara 5 EPL, mara 2 Kombe la Ligi.

ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0

 

Soma na hizi

Tupia Comments