Serikali kupitia wizara ya Maliasili na utalii imeanza zoezi la kufunga redio maalum za mawasiliano wanyama wakali ,waharibifu na wanyama mbalimbal lengo upatikanaji wa taarifa za wanayama hao katika masuala ya ulinzi na ujangili zoezi ambalo limefanyika katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi wilayani kilosa mkoani Morogoro
Waziri wa maliasili na Utalii Balozi Dokta Pindi Chana ameongoza zoezi hilo ambapo amesema siku za hivi karibuni kumekua na changamoto ya wanyama wakali kama Tembo kuvamia mashamba ya watu na kuharibu mali na kuuwa hivyo redio hizo zitakua na uwezo wa kuonesha mahali wanyama hao walipo ili iwe rahisi kuwadhibiti.