Leo ndio ile siku ambayo wabunifu mbalimbali kutoka Tanzania waliweza kuonyesha kazi zao kupitia tamasha la VAA Africa Festival Arusha 2017 likiwa ni Tamasha jipya la mitindo ya mavazi Tanzania ambalo limeanzishwa kwa lengo la kuinua wajasiriamali chipukizi wabunifu.
Kupitia maonyesho hayo wabunifu wanaweza kutangaza kazi zao na kupata nafasi ya kukutana na watu mbalimbali waliofanya vizuri kwenye soko la ubunifu ndani na nje ya Tanzania. Tamasha hilo limeanzishwa mwaka huu ambapo litakuwa linafanyika mara tatu kwa mwaka katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.
Hapa nimekusogezea stori picha kutokea Mount Meru Hotel Arusha ambapo maonyesho haya yamefanyika
Video: Watanzania walioajiri Wajerumani kujenga kiwanda cha Dawa cha kisasa Bagamoyo>>>