Moja ya story ambayo inamake headlines kwa sasa katika mitandao mbalimbali ni kuhusu kesi inayowakabili Rais wa TFF Jamal Malinzi na wenzake wawili ambao wanakabiliwa na mashtaka 28.
Leo July 5, 2017 Wakili wa kujitegemea, Jerome Msemwa amejitoa katika kesi Namba 213 ya 2017 inayowakabili Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo Mwanga.
Msemwa ambaye alikuwa akiwatetea washtakiwa hao, ameandikia barua kwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri leo July 5, 2017 akieleza amejitoa katika kesi hiyo kutokana na kutopata maelekezo sahihi kutoka kwa wateja wake.
VIDEO: Kutoka TAKUKURU Rais wa TFF Malinzi na Katibu Mkuu wanashikiliwa!!!