Usiku wa Mei 2 2016 kuamkia Mei 3 2016 ulikuwa ni usiku wa kihistoria katika soka la Uingereza, tunaweza kuita ulikuwa usiku wa kihistoria kutokana na Ligi Kuu Uingereza kufanikiwa kupata Bingwa mpya wa mashindano hayo tofauti na miaka iliyopita tulizoea kuona vilabu vya Man United, Liverpool, Chelsea, Man City na Arsenal vikitawala.
Leicester City imefanikiwa kutangaza Ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza huku ikiwa na michezo miwili mkononi, Leicester City ilikuwa itangazwe Bingwa wa Ligi Kuu jana kama ingefanikiwa kuifunga Man United, lakini kwa bahati mbaya mchezo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, kitu ambacho kilifanya kusubiri matokeo ya Chelsea dhidi ya Spurs.
Sare ya 2-2 kati ya Tottenham Hotspurs dhidi ya Chelsea ndio iliyosababisha Leicester City kutangazwa Mabingwa wa Ligi Kuu, licha ya kuwa Chelsea walianza kufungwa goli mbili za mapema, wachezaji wa Chelsea wakipewa sapoti ya mashabiki wao walifanikiwa kujituma kama wanatafuta Ubingwa na kusawazisha.
Magoli ya Chelsea yalifungwa na Gary Cahill dakika ya 58 na Eden Hazard ndio alifunga goli la kusawazisha dakika ya 83. Magoli ya Chelsea yalifungwa kipindi cha pili baada ya Harry Kane kupachika goli langoni kwa Chelsea dakika ya 35 na Heung-Min Son kufunga goli dakika ya 54.
Video ya magoli Chelsea vs Leicester City, Full Time 2-2
https://youtu.be/a19gwIHqsR0
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ALL GOALS: AZAM FC VS ESPERANCE (FULL TIME 2-1) APRIL 10 2016
https://youtu.be/duzv5kA8Q-c