Septembe 30 2015 beki wa kati wa zamani wa Simba aliyekuwa anaichezea Mbeya City wakati huo Juma Nyosso alifungiwa na TFF miaka miwli kutokucheza soka ikiwa ni adhabu ambayo amepewa baada ya kumfanyia kitendo kisichokuwa cha kiuungwana John Bocco.
Adhabu ya Juma Nyosso ya kufungiwa miaka miwili kucheza soka ilikuja baada ya kurudia kufanya kosa hilo kwa mara tatu tofauti akiwa amewahi kumfanyia kitendo hicho pia Elias Maguli wakati akiwa Simba na amewahi kumfanyia hivyo pia mshambuliaji wa zamani wa Simba Joseph Kaniki mwaka 2007 wakati Nyosso akiwa Ashanti United.
Jana June 14 ikiwa ni siku moja kabla ya dirisha la usajili la wachezaji soka Tanzania kufunguliwa, club ya Kagera Sugar ya Bukoba ilitangaza kuingia na Nyosso mkataba wa mwaka mmoja, adhabu ya Juma Nyosso kwa kawaida itaisha mwezi Septemba vipi kanuni zinasemaje?
“Tumeona kwenye mitandao ya kijamii Kagera Sugar wakitangaza kumsajili Juma Nyosso naamini Kagera Sugar watafuata taratibu za usajili, huyu ni mchezaji ambaye ana adhabu ya kufungiwa miaka miwili lakini kubwa ni kuwa Nyosso ameleta barua TFF ya kuomba radhi”>>> Alfred Lucas
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera