Mara nyingi watu wanaposhindwa na jambo hukata tamaa lakini kushindwa mara moja haimaanishi huwezi kufanikiwa jambo hilo ukijaribu tena na tena, leo nimekuletea list ya wanamuziki kumi waliowahi kuambiwa hawajui kuimba na leo hii ni mastaa wakubwa duniani.
1: Beyonce.
Akiwa na miaka 14 tu alipelekwa na baba yake Mathew Knowles studio lakini producer alipomsikia Beyonce akiimba alimwambia hadhani kama kuimba ni kipaji chake lakini leo hii Beyonce ni miongoni mwa waimbaji wakubwa duniani akiwa na thamani ya zaidi ya dola za kimarekani Milioni 600 na kuuza zaidi ya rekodi milioni 34.
2: Shakira.
Shakira ni miongoni mwa waimbaji wenye mafanikio makubwa dunia akiwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 220 na kuuza rekodi zaidi ya milioni 60 duniani kote lakini aliwahi kukataliwa kujiunga na kikundi cha kuimba kwaya kanisani na mwalimu wake wa muziki kumwambia ana sauti mbaya inayofanana na mbuzi.
3: Spice girls.
Spice girls ni moja ya kundi la muziki lililojipatia umaarufu mkubwa miaka ya 90 kwa kuuza zaidi ya rekodi milioni 85 duniani kote, lakini waliwahi kuambiwa na producer maarufu Simon Cowel kuwa hawatafika popote kimuziki na ana washauri waachane na muziki na kutafuta kazi nyingine.
4: One Direction.
One Direction ni kundi linalopendwa duniani na wamepata mafanikio makubwa kimuziki lakini mwanzoni mwa carrier yao waliposhiriki shindano la kutafuta vipaji la xfactor waliwahi kuambiwa na Jaji wa shindano hilo kuwa hadhani kama wanaweza kufika mbali kimuziki lakini leo ni miongoni mwa kikundi kilichojiandikia historia ya kuwa kwenye list ya Forbes na kua bendi inayolipwa fedha nyingi duniani kwa mwaka 2014.
5: Lady Gaga.
Kwa mara ya kwanza aliposainiwa na label ya L.A. Reid ya Def Jam mwanamuziki Lady gaga aliwahi kuambiwa na producer wake kuwa muziki wake unakera sana masikioni na hadhani kama muziki ni kipaji chake lakini leo hii Lady gaga ni miongoni mwa wanamuziki waliouza zaidi ya rekodi milioni 10.3 .
6: Madona.
Baada ya kuacha chuo akiwa na miaka 17 tu Madona alikwenda jijini New York kujiendeleza kimuziki akiwa na dola 35 tu mfukoni lakini muziki wake ulikataliwa waziwazi na aliyekuwa Raisi wa Millennium Records Jeremy Ienner na kumwambia hamwelewi anachoimba na hadhani kama anaweza kuja kuwa mwanamuziki mzuri.
7: Jordin Spark
Jordin Spark ni mshindi wa shindano la kutafuta vipaji American Idol mwaka 2006 na kuibuka mshindi lakini hakupata ushindi huo na kuwa mwanamziki mkubwa leo hii kiurahisi, aliwahi kukataliwa na majaji wa shindano hilo zaidi ya mara mbili lakini hakukata tamaa alirudia tena na akaibuka mshindi wa shindano hilo .
8: Hillary Scot.
Ni mwanamuziki wa nyimbo za Country ana jumla ya tuzo 7 za Grammies ana thamani ya dola million 11 na kuuza jumla ya rekodi milioni 18 duniani kote, kabla ya kuwa mwanamuziki mkubwa Hillary Scot alikataliwa na maproducer wa show ya American Idol na hakupata hata nafasi ya kufika kwa majaji wa shindano hilo.
9: Mary Lambert.
Akiwa na miaka 16 Mary Lambert alishiriki shindano la kutafuta vipaji la American Idol lakini producer wa kipindi hicho Ryan Seacrest alimwambia hadhani kama aina ya uimbaji wake unafaa hata kuingia mzunguko wa kwanza washindano hilo na kumwambia aondoke.
10: Tori Kelly.
Tori Kelly ni mwanamuziki aliyemfanya Jaji wa American Idol Simon Cowel kujutia sana uamuzi wake wa kumtoa kwenye shindano hilo, kwani miezi michache tu baada ya kutolewa kwenye shindani Tory Kelly alitumia mtandao wa Youtube kuonesha kipaji chake.
VIDEO:Ulimiss hii show ya bonyeza play video hapo chini.
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo