Story ya kwanza kusikila kwenye 255 ya leo february 20, inahusu taarifa zilizosambaa jana kwenye mitandao ya kijamii kuwa Clouds Media Group imeuzwa na imenunuliwa na mfanyabiashara Rostam Aziz.
Akizungumzia ishu hiyo Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema kuwa kuna watu wanaitumia vibaya mitandao ya kijamii ndio walioandika kuhusu ishu hiyo, amesema Clouds imejengwa kwa jasho kuanzia chini hadi hapo ilipo, taarifa za kuuzwa hazina ukweli wowote na hata wangeamua kuuza ingekuwa ni kibiashara.
Kusaga amesema ni kampuni nyingi wametaka kuinunua Clouds lakini hawako tayari kwa kuwa wanaweza kuendelea wenyewe.
Msanii Diamond Platnumz amesema kuna watu wameizungumzia tofauti ishu ya yeye kutoonekana kwenye msiba wa baba wa Dully Sykes mzee Ebby Sykes.
Amesikika kwenye 255, Diamond amesema kwa sasa yuko katika kipindi ambacho sio kizuri kwake na familia yake lakini hawezi kuzungumza kila kitu, mama yake anaumwa sana na kwa sasa yuko kwenye matibabu India, Dully ni kama kaka yake aliyemsaidia vitu vingi sana na Mzee Sykes ni kama mzazi wake ambaye ana mchango pia kumfikisha hapo alipo sasa.
Diamond amesema alitoa pole ya msiba kwa Dully.
Story ya mwisho kusikika ni taarifa ya msiba wa aliyekuwa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Mez B ambaye amefariki Dodoma baada ya kuumwa kwa muda mrefu.
Noorah amesema Mez B alikuwa na homa tangu mwezi December mwaka jana na baadaye akasafiri kwenda Dodoma huku hali yake ikiwa bado sio nzuri, mara ya mwisho wameongea kwenye simu ni siku tano zilizopita, leo simu yake imepokelewa na dada yake akimtaarifu kuwa Mez B amefariki muda mfupi uliopita baada ya kuzidiwa.
Bonyeza play hapa uisikilize story zote.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook