Msanii Mo Music amesema kuwa ameamua kuwekeza kwenye biashara ya kuuza senene na dagaa ili kuongeza vyanzo vya mapato yake baada ya kutegemea muziki peke yake, hana muda mrefu sana lakini tayari Mikoa ya Dar, Mwanza na Morogoro imekuwa na soko kubwa la biashara yake.
HK ambaye ni meneja wa msanii Snura amesema kwa sasa msanii huyo yuko kwenye maandalizi ya kutoa wimbo wake ambao utatoka mwezi wa pili mwaka huu baada ya kutoonekana na kwenye stage kwa zaidi ya miezi sita.
Kulienea story za msanii Ray C kwamba ameacha kutumia tiba ya methanol ambayo amekuwa akitumia kumtibu kutokana na kuathirika na dawa za kulevya lakini msanii huyo ameongea na 255 na kusema sio kweli kwamba ameacha tiba hiyo kwa kuwa ripoti ya daktari inaonyesha yeye ni mmoja wa wagonjwa ambao wanaendelea vizuri na matibabu hayo.
Jimmy Lovine na Dr. Dre wameshitakiwa na Kampuni ya Monster ambao wamelalamika kwamba wameibiwa teknolojia na Kampuni ya Beats mwaka 2008 wakati waliposhirikiana kutambulisha bidhaa ya headphones hizo kabla ya mkataba wao kuvunjika 2012.
Isikilize 255 yote hapa kwa kubonyeza play.
Nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitterInstaFacebook