Jamaa ambaye aliibua shangwe za watu wengi alipopanda kwenye stage ya #AfterSkulBash, mwezi December, 2014 pale Escape One, ambapo shangwe za watu hao zilitokana na jinsi jamaa huyo Mohammed Said aka Ngwea Jr alivyofanana na Marehemu Albert Mangwea, ameelezea mikakati yake ambapo mpaka sasa amesharekodi nyimbo kadhaa ili kuingia rasmi kwenye game.
Ngwea Jr. amesema washkaji zake waliosikiliza nyimbo zake wameifananisha sana sauti yake kwenye nyimbo hizo na ya Marehemu Ngwea, Mohammed amesema kuwa ameamua hivyo kama njia ya kumuenzi msanii Mangwea.
Mwaka jana kulikuwa na mfululizo wa nyimbo nyingi za wasanii Tz kuvuja, Diamond Platnumz ni mmoja ya wasanii ambao nyimbo zao zimevuja pamoja na Yamoto Band ambapo Mkurugenzi wa Kundi hilo Said Fella amesema lengo lao kurekodi nyimbo zao ni kwa ajili ya mashabiki wao kusikiliza na hawajawahi kuvujisha nyimbo za kundi hilo makusudi.
Rapper Stereo ameamua kurudia nyimbo kadhaa za wasanii mbalimbali kutokana na kwamba wasanii hao walikuwa wakimvutia kabla hajatoka, akaamua kufuata njia zao na kuanza kuimba pia, nyimbo ambazo amezungumza tayari na wenye nazo kwa ajili ya kuzirudia ni pamoja na wimbo wa AY (Usijaribu), Fid Q (fidq.com) Chid Benz (Kama Unaweza) Mwana FA (Binamu) na Joh Makini (Muda), iwapo akikubaliana na wasanii wengine kurudia nyimbo zao ataandaa album ya nyimbo zote atakazozirudia.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook