Msanii wa Bongo Flava AT amezungumzia maneno magumu ambayo amekuwa akiyatumia kwenye nyimbo zake na kusema maneno anayoyatumia ni haya ya Kiswahili, lakini kwa sababu watu wanatumia sana swaga ndio maana wanapata ugumu, kama neno alilotumia kwenye wimbo wa Flora Mvungi lakini ni neno la kawaida ila kwa sababu halitumiki sana watu wanaona ni neno gumu.
Baada ya msanii Kala Jeremiah kuweka kava la wimbo wake mpya kwenye Instagram unaoitwa ‘Nchi ya Ahadi’ aliomshirikisha Roma Mkatoliki na kuzua maswali mengi, 255 imepiga nae story kujua kwanini ameamua kuuita jina hilo ambapo amesema ni kwasababu ni jambo linalowahusu wa Tanzania wote na siku atapouachia kila mmoja autafute kwa sababu, atakuwa na kitu cha kujifunza kwenye wimbo huo na ameamua kumshirikisha Roma kwasababu ulikuwa ni muda muafaka tofauti na awali ambapo walikuwa na majukumu mengi.
Info ya mwisho kusikika inahusu taarifa zilizochukua headline jana kwenye vyombo vya habari juu ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, baada ya kutolewa kwa hukumu ya kesi aliyokuwa ameifungua kupinga CHADEMA kujadili uwanachama wake, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lisu amesema, wamemshinda kesi aliyofungua na kutokana na katiba ya chama hicho Zitto sio mwanachama wa chama hicho tena.
Wakili za Zitto, Alberto Msando amesema kilichotokea sio hukumu kwasababu kesi ya msingi bado haijasikilizwa, ila kulikuwa na mapingamizi ya awali kuhusu uhalali wa kesi ya msingi kuwepo mahakamani ndicho kitu Mahakama imetolea maamuzi kwamba, pingamizi la awali linamantiki kuwa kesi hiyo ilitakiwa ifunguliwe Mahakama ya chini na sio hukumu kama inavyosemekana kwa kuwa, kesi ya msingi bado haijasikilizwa na hawakuwa na taarifa za kesi hiyo kusomwa jana, kwa sasa wanaangalia nini cha kufanya ili waweze kujiridhisha, kuhusu kuvuliwa uwanachama wake amesema tamko hilo limewasikitisha na halijafata utaratibu lakini kunauwezo wa kupeleka swala hilo Mahakamani na kuomba zuio la muda hadi kesi itakaposikilizwa ili aendelee kuwa mwanachama.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook