Leo Novemba 28 kwenye 255 ya XXL, Miss Info karipoti story kadhaa zinazowahusu mastaa mbalimbali.
Story ya kwanza kusikika kwenye 255 ya leo ni ile inayomuhusu msanii AY ambae wiki hii ameingia kwenye list ya wasanii waliofanya fanya kolabo na wasanii wakubwa Duniani ambapo hivi karibuni alishirikiana na nyota wa kimataifa Sean Kingstone kwenye kolabo yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Touch Me’ akimshirikisha Sean Kingstone ngoma iliyoirekodia kwa Producer anaetengeneza ngoma za Beyonce na Lady Gaga.
AY amefunguka sababu ya ngoma hiyo kuchelewa kutoka licha ya kufanywa siku nyingi, ni kutokana na kuwa busy na mambo kuingiliana pia kutaka video ya ngoma hiyo itoke sambamba na audio, video hiyo ambayo aliifanyia nyumbani kwa Sean Kingstone Marekani kutokana na urafiki wao, Ay amezungumzia swala la kurudia rudia kolabo na Miss Trinity na kusema ni kwa sababu ya kufanya kazi katika lebo moja ya Cheki My Slash Network Show Busy Calfonia, ambao wapo wasanii watatu Ay, Miss Trinity na Mamae waliokutana mwaka 2008, akiendelea kufunguka Ay amezungumzia maneno yaliyoenea kuhusu kurudi kwa kundi la East Cost Team yeye akiwa mmoja kati ya wasanii waliokuwa wanaounda kundi hilo kukaa pamoja kwa miezi kadhaa na kufanya project ya pamoja ikiwemo kurudia Hits za ngoma zao walizowahi kuzifanya vizuri kama Komaa nao, Ama zangu ama zao na nyingine project inayotegemea kuanza Januari 2015 na kila mtu anashauku kubwa ya kufanya kazi kwa pamoja.
Msanii OMMY DIMPOZ leo ameachia Video ya ngoma yake ya Tupogo Remix na kuanzia jumatatu ijayo kupitia akanti zake za mitandao ya kijamii Instagram, Facebook na Twitter ambazo anatumia jina la @ommydimpoz atakuwa anaendesha shindano la kuchezesha ngoma hiyo inayoitwa Lima na Tupogo, ambalo kila mwisho wa wiki mshindi atakuwa anapewa shilingi laki tano, shindano linalotokana na kionjo kilichokuwepo kwenye nyimbo hiyo cha limalima, shindano hilo litadumu kwa mwezi mmoja na lengo la shindano hilo ni kuwaomba radhi mashabiki kwa kuchelewa kutoa Video ya Tupogo na anategemea kutoa Albam siku ya Valentine day.
Bungeni Dodoma bado kunawaka moto baada ya sakata la akaunti ya ESCOR kuibuliwa na Mbunge David Kafulila baada ya kamati ya mahesabu ya PAC kusoma repoti iliyofanyika na uchunguzi ukaonyesha kuna ujanja uliofanyika kukwarua mabilioni ya shilingi kutoka Tanesco kwenda kwenye akaunti ya ESCROW ripoti iliyotaja baadhi ya majina ya viongozi waliohusika katika sakata hilo.
Haya ni maoni ya baadhi ya Wasanii waziozungumza ndani ya 255
BONTA amesema kwa maoni yake yeye anahisi anachokiona baada ya ripoti kuja ni kuwa toka kuanza kwa uchangiaji wa ile ripoti kuanzia jana hadi leo, anachokiona ni uchangiaji wa ile ripoti sio wa facts ya ile ripoti yenyewe uchangiaji umekuwa ni wakichama na Watanzania wengi hawajui ukweli wa picha halisi ilivyo, Raisi wetu kwa miaka kumi kasoro kashavunja Baraza la Mawaziri zaidi ya mara tatu na kama hili sakata likionekana kama ni kweli Baraza la Mawaziri litavunjwa na Waziri Mkuu pia atajiuzulu swala amabalo litazidi kuwachafulia.
KALAPINA nae akatoa mawazo yake kuhusiana na sakata hilo amesema kwa maoni yake zile ni pesa za Umma kwa hiyo wahusika inabidi wafilisiwe Mali zao na wapelekwe Mahakamani ili kujibu tuhuma zinazowakabili, jambo ambalo kwa upande mwingine watu wanajikuta wakipandishiwa gharama za vitu kila siku kama Umeme unit moja shilingi miatano madeni ambayo yanafanywa na mafisadi wachache na mwisho wa siku yanakuja kumwangukia mwananchi wa kawaida.
Bonyeza play hapa kuisikiliza
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook