‘Marehemu Kaacha Orodha’ ni jina la album ya mwisho kuiachia msanii Jebby, baada ya hapo kumekuwa na ukimya wa miaka saba ambapo anasema familia yake walikaa na kumshauri kwamba afanye mambo mengine kwa kuwa hawakuonna kama muziki unamlipa.
Kwa muda wote amesimama kufanya muziki kutokana na dada yake ambaye amemlea toka toka akiwa mdogo kumshinikiza afanye hivho japo aliendelea kurekodi bila wao kujua.
Wasanii wa kike TZ wameungana na kufanya wimbo wa kulaani mmauaji ya albino, msanii Keisha amesema wamefanya vitu vingi kwa kuwashirikisha wanaume hivyo kwenye hii wameamua kusimama wenyewe kuonesha kwamba wanaweza.
Baadhi ya walioshiriki ni pamoja na Shamsa Ford, Keisha, Linah, Mwasiti, Shilole, Kajala na Jackline Wolper.
Msanii Keisha amesema hajawahi kukutana na dalili za tukio la kutishiwa lakini anahisi kwa hali ilivyo wakati wowote inaweza kumtokea na hata ndugu zake wamekuwa na hofu ya hilo.
Keisha amesema anaamini kwamba wanaojihusisha na vitendo hivyo inatokana na kukosa elimu, uelewa pamoja na tamaa.
Bonyeza play uisikie hapa yote…
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook