Kwenye 255 ya XXL Clouds FM February 25 2016 stori za burudani zilizochukua nafasi ni pamoja na hii ya Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds MEDIA Ruge Mutahaba kuongelea Fursa 10 kupiti 360 ya Clouds TV.
‘katika kitabu nilichokuwa na kisoma na ripoti ya World Economic Forum kwa Afrika Media Entertaiment ilikuwa ni namba 1, mimi nimeiweka namba nne kwa hapa Tanzania nimeweka namba 4 kwasababu nadhani bado kuna vitu amabavyo bado hatujavifikia kutuwezesha kuwa namba 1‘
‘Kama tutaanza kutengeneza mfumo wa kutuwezesha sisi kufanya biashara, ni soko kama china, India ilivyo kuwa na bollywody ndio maana kwa sasa hivi tunaiona ni indrust kubwa yenye nafasi kubwa sana ya kupanuka‘>>> Ruge MutahabaStori nyingine ni hii ya wimbo ya ‘make me sing‘ ya Diamond Platinumz kufananishwa na video ya Lil Wayne ‘Got Money‘ ambapo Diamond amejibu >>> ‘watu wanashindwa kuelewa kila kitu ambacho kinafanyika katika muziki sasa kwenye video, kwenye kuimba, mashairi na vyote vilishafanyika, vimeshaimbwa ni kama marudio lakini kila mtu anarudia kwa namna yake anayoijua yeye’
Ya amwisho ambayo imesikika kwenye 255 ni hii ya rapper wa bongofleva Edu Boy kawashangaza wengi baada ya kuachia mdundo wake mpya kwa style ya kuimba tofauti na watu walivyomzoea kwamba siku zote yeye ni mtu wa michano.
Amehojiwa na kusema >>> ‘Unajua Edu Boy sitaki kubaki hapa inabidi jina liendelee kukua profile ikue niwe wa kimataifa na sio nibaki tu local so ili nikue inabidi nifanye vitu vingi ambavyo ni tofauti, nina nyimbo nyingi za kuimba nimezifanya sema kwa kutoa huu ndio unakua wa kwanza’
Kama unazitaka stori zote kutoka 255 kwa ukamilifu zikiripotiwa na Perfect Crispin, bonyeza play kwenye hii audio hapa chini…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagramna YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE