Najua time ambayo XXL iko hewani kuna watu mko busy na mambo mengine, mnakosa kabisa time ya kusikiliza story zilizo kwenye headlines za kiburudani.. ninachokifanya ni kuzirekodi na kukuwekea hapa ili usipitwe kabisa mtu wangu.
#255 ilikuwa na story ya kwanza ya rapper toka Mji kasoro Bahari, Stamina ambae amesema kwamba baada ya kusikiliza mfululizo wa track zake nyingi kwa zaidi ya miaka minne kaamua May 30 2015 kuachia album yake rasmi kabisa !!
Stamina kasema album itakuwa na ngoma kama 20 hivi, uzinduzi utafanyika Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri.. watu wake wakae tayari kwa burudani toka kwa list kubwa ya mastaa ambao watamsindikiza kwenye show hiyo.
Ally Dax ni Mtanzania mwanamitindo ambaye anafanya poa kwenye industry hiyo South Africa.. Jamaa kasimulia kwamba tangu ameanza kufanya show za mavazi Afrika Kusini kiasi kidogo cha pesa ambacho aliwahi kulipwa ni kama laki 3 za TZ.. lakini Bongo kiwango cha chini alilipwa elfu 30 na kiwango cha juu ni laki 1 na nusu.
Dax amesema South Africa kuna ubaguzi wa models wakiwa backstage kwenye show, huwa hakuna usawa jinsi ambavyo wanachukuliwa models wa nchi nyingine.
Staa mwingine wa muziki Young Suma amesema video ya ‘Hatujivungi‘ ilikuwa ikamilike muda mrefu lakini kukatokea vitu ambavyo vikafanya video kutokamilika kwa wakati.. kaamua kuitimiza ahadi yake, amesema video imekamilika na ataandaa party kwa ajili ya uzinduzi maeneo ya Mikocheni.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.