Karudi na kasikika tena kwenye HEADLINES za burudani, msanii wa kundi la Navy Kenzo na producer wa hit kibao Bongo Flevani, Nahreel amesema hajawahi kuondoka na beats za kundi la Pah One kama ambavyo wasanii wa kundi hilo wanadai.
Story yake ni moja ya zilizoko kwenye #255, jamaa anasema aliondoka na vitu vyake ikiwemo beats alizotengeneza mwenyewe na alikuwa nazo hata kabla hawajaanzisha kundi hilo, wao kama kundi hawana mpango wa kufanya collabo na Pah One.
Staa wa muziki Bongo anaewakilisha Mwanza Mo Music leo ameachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Nitazoea’.
Mo Music amesema ujumbe wa wimbo huo unahusu watu ambao wamewahi kuumizwa.. YES, ni ujio wake mwingine Bongo Flevani, anategemea wimbo huu utafika mbali kama wimbo wa ‘Basi Nenda’ ulivyomtoa.
Collabo ya ‘Raha’ ya mkali mwingine wa DAR, Bill Nas Feat. Nazizi & TID ni hit kwenye chati ya muziki.. Bill amesema ameamua kutumia nafasi aliyonayo kwa kujitolea kumsaidia mtoto mwenye ulemavu wa ngozi anayeitwa Princess, jamaa kaamua kumlipia ada ya miaka miwili mtoto huyo.
Hela ambayo Bill kamlipia ada Princess ni sehemu ya aliyoipata kupitia muziki wake.
Zilikupita zote mtu wangu? Nilirekodi na kukusogezea hapa mtu wangu.. Bonyeza play uzisikie
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook