Zilizonifikia leo kutoka kwenye meza ya 255 ni pamoja na stori kutoka Yamoto Band, Meneja wao amesema video ya wimbo wao mpya wa ‘Cheza kwa Madoido’ imetumia kiasi cha dola 15,000 zilizotolewa na Diamond, amesema haikuchelewa kuonyeshwa MTV Base kwa kuwa wana mipango yao.
Sheria ya makosa ya mitandao imeanza jana.. lakini kuna watu hawajaridhika na maamuzi hayo..Msanii wa HipHop Bonta amesema si rahisi watu kubadili tabia kwa haraka, na hii sheria imekuja wakati mpya wa siasa ambao watu wamekuwa wakibishana sana kuhusu siasa.,,wangetoa muda kwanza watu waelimishwe.
Pia Nick Wa Pili naye amezungumza na kusema matumizi ya mitandao lazima yazingatiwe na kusimamiwa, anakubaliana na sheria hiyo lakini uhuru wa kuzungumza usiingiliwe.
Nahreel amezungumzia kifo cha msani aliyetoka kwenye kundi lao la Pah One, Shikizi, amesema alikua mtu wao wa karibu sana kwa kuwa walifanya kazi kwa ukaribu na alikufa wakati akiogelewa katika kisiwa cha Mbudya.
Wasikilize hapa..
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos